1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa ameuliwa Darfour

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxm

Addis Ababa/New York:

Mwanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa ameuliwa katika mkoa wa machafuko wa Darfour.Maafisa wa Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa wamesema mwanajeshi huyo wa kulinda amani ambae ni raia wa Misri ameuliwa na maharamia waliokua na silaha walioivamia na kupora nyumba yake.Hii ni mara ya kwanza kwa msimamizi wa amani wa Umoja wa mataifa kuuliwa tangu jumuia ya kimataifa ilipoamua kusimamia amani katika jimbo hilo lililoteketezwa kwa vita-Darfour.Umoja wa Afrika umetuma wanajeshi elfu sabaa katika jimbo hilo.Umoja wa mataifa unajitahidi kutaka idadi ya wanajeshi hao iongezwe na kufikia watu 22 elfu pakiwepo zowezi la pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuwalinda raia wa kawaida na kutumia nguvu ikilazimika kuzuwia matumizi ya nguvu.Rais Omar el Bashir wa Sudan hadi wakati huu alikua akipinga fikra kama hiyo.