1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamgambo wa Tamil Tigers ajiripua Sri Lanka

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CU87

Nchini Sri Lanka,mshambulizi wa kujitolea muhanga wa kundi la waasi la Tamil Tigers amejiripua mbele ya ofisi ya Waziri wa Ustawi wa Jamii, katika mji mkuu Colombo.Waziri Douglas Devanand wa kabila la Kitamil amenusurika,lakini katibu wake ameuawa na watu 2 wengine wamejeruhiwa. Shambulizi hilo limefanywa siku moja baada ya mkuu wa Tamil Tigers,Velupillai Prabhakaran kusema kuwa hana matumaini ya kupata suluhisho la kisiasa kuhusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe kisiwani Sri Lanka.