1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamke mzito kabisa duniani kufanyiwa upasuaji

Sudi Mnette
15 Februari 2017

Yule anaeaminika kuwa mwanamke mnene kabisa duniani amewasili nchini India kwa ajili ya upuasuaji wenye lengo la kupunguza uzito wake.

https://p.dw.com/p/2XcjV
Ägypten Eman Ahmed,  die schwerste Frau der Welt
Picha: picture-alliance/dpa/Family Handout

Madaktari wameanza maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa dharura kwa kumnywisha kimiminika kitakachomwezesha kupunguza uzito. Hatua hiyo inatokana na waziri wa mambo ya nje kuingilia na kutoa ahadi ya kufanikisha upatikanaji wa visa kwa ajili ya safari hiyo. Eman Ahmed Abd El Aty, mwenye umri wa miaka 36, anakadiriwa kuwa na kilo 500. Kutokana na umbo lake amesafiri katika nafasi maalumu ya ndege iliyotengenezwa kwa ajili yake. Hivi karibuni dada wa bonge huyo, alimwendea dokta Lakdawala na kumweleza kuwa ndugu yake anahitaji huduma ya dharura ya matibabu. Alikuwa anavimba viungo vyake na kuandamwa na maradhi mengine ya moyo na sukari. Safari ya Eman imekuwa changamoto kubwa na hasa kwa kuzingatia umbile lake lililomfanya hasindwe kujongea au kutembea na kusalia ndani ya nyumba kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Wachunguzi wa mambo wanasema kama uzito wa Abd El Aty utathibitika basi atakuwa kavunja rekodi iliyowekwa na Pauline Potter wa Marekani ambae alikuwa na uzito wa pauni 643, na kufanya awe na rekodi ya mwanamke mwenye uzito wa juu kabisa aliye hai. India imekuwa kivutio kikubwa kwa kutoa tiba bora na nafuu ikilinganishwa na mataifa ya Magharibi.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman