1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha Oscar Pistorius nguvuni

14 Februari 2013

Mwanariadha nyota wa Afrika kusini katika michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya walemavu Oscar Pistorius, ametiwa nguvuni leo(14.02.2014) baada ya mpenzi wake wa kike kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Pretoria.

https://p.dw.com/p/17dsa
South Africa's Oscar Pistorius starts his men's 400m round 1 heats at the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium August 4, 2012. REUTERS/Dylan Martinez (BRITAIN - Tags: OLYMPICS SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Oscar Pistorius katika michezo ya olimpiki mjini LondonPicha: Reuters

Oscar Pistorius maarufu kama "mkimbiaji anayekimbia na miguu ya chuma", anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo(14.02.2013).

Polisi ya Afrika kusini ilijizuwia kumtaja Pistorius mwenye umri wa miaka 26 kuwa ni mtuhumiwa wa mauaji hayo, lakini imethibitisha kuwa mwanamke mmoja amekutwa amefariki katika eneo la Silver Wood mashariki ya mji huo mkuu.

Oscar Pistorius of South Africa looks on as he walks before the men's 400 meters event at the 23rd International Athletics Meeting in Lignano Sabbiadoro July 17, 2012. After striving to qualify for the 400 metres at the London Olympics for six years, Oscar Pistorius believes he will now be better placed to run at the Rio de Janeiro Games in 2016. The South African, who wears carbon fibre blades, will become the first double amputee to compete in the Olympics. REUTERS/Alessandro Garofalo (ITALY - Tags: SPORT ATHLETICS OLYMPICS)
Oscar PistoriusPicha: Reuters

Polisi imesema kuwa Pistorius aliwekwa korokoroni baada ya kutokea mashambulizi hayo mapema leo asubuhi. Luteni kanali Katlego Mogale ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa polisi ilipokea simu mapema leo asubuhi (14.02.2013) kuwa kulikuwa na mashambulio ya risasi katika nyumba anayoishi mwanariadha huyo ambaye miguu yake yote imekatwa.

Maafisa wa polisi walikuta bastola katika eneo la tukio na kumchukua mwanariadha huyo na kumuweka korokoroni. Afisa huyo wa polisi amesema kuwa wakati polisi walipowasili walimkuta mwanariadha huyo akijaribu kumpa msichana huyo huduma ya kwanza kwa nia ya kumrejeshea uhai. Mogale amesema Pistorius alikuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye leo mchana.

Vyombo vya habari

Vyombo vingi vya habari nchini Afrika kusini vinaripoti kuwa mwanamke huyo aliyeuwawa alikuwa mpenzi wake Pistorius na kwamba huenda alidhania kuwa ni mwizi na kumpiga risasi, lakini polisi hawajafafanua uhusiano wa mwanamke huyo na Pistorius.

Oscar Pistorius (C) of South Africa competes in the men's 400M - T44 category at the National Stadium, known as the 'Birds' Nest' during the Beijing 2008 Paralympic Games, China, 16 September 2008. Pistorius won with a new world record time of 47.49 seconds. EPA/DIEGO AZUBEL +++(c) dpa - Bildfunk+++
Pistorius katika michezo ya walemavuPicha: picture-alliance/dpa

Pistorius aliandika historia katika michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana wakati alipokuwa mtu wa kwanza ambaye miguu yake imekatwa kushindana katika mbio fupi katika michezo hiyo mjini London, na ni mmoja kati ya wanariadha maarufu kabisa barani Afrika.

Kutokana na kukatwa miguu yake kuanzia magotini wakati akiwa na umri chini ya mwaka mmoja, alifanya kampeni kwa miaka kadhaa kuruhusiwa kushindana dhidi ya wanariadha ambao hawana ulemavu na hatimaye aliruhusiwa na mahakama ya juu ya michezo kushindana katika michezo mbali mbali.

epa02884536 Oscar Pistorius from South Africa (L) and Femi Ogunode from Qatar (R) compete in the mens 400m round 1 during the 13th IAAF World Championships in Daegu, Republic of Korea, 28 August 2011 EPA/KERIM OKTEN
Oscar Pistorius (kushoto)Picha: picture alliance/dpa

Bingwa wa mbio za walemavu

Alishiriki katika mbio za mita 400 na pia katika kikosi cha Afrika kusini kinachokimbia mbio za mita 400 kupokezana vijiti katika mashindano ya Olimpiki mjini London na pia alishinda tena katika mbio za mita 400 za walemavu katika michezo ya Olimpiki mjini London.

Hata hivyo alishindwa kurejesha taji lake la mbio za mita 200 kwa walemavu kwa kushindwa kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka tisa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape /

Mhariri:Josephat Charo