1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha wa Kenya ashinda mbio za mita 3,000

Admin.WagnerD6 Agosti 2012

Mwanariadha wa Kenya, Ezekiel Kemboi, pamoja na kukabiliwa na mashtaka nchini mwake, aliyaweka kando hayo na kudumisha jitihada za taifa lake katika ushindi wa mbio za mita 3,000 katika michezo ya Olimpiki huko London.

https://p.dw.com/p/15kZu
Kenya's Ezekiel Kemboi poses after winning the men's 3000m steeplechase final during the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium August 5, 2012. REUTERS/David Gray (BRITAIN - Tags: OLYMPICS SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Ezekiel KemboiPicha: Reuters

Mambo yalianza namna hiyo hapo jana, mtangazaji akitaka kila mmoja atayarishe tiketi yake tayari kwa ukaguzi kabla kuingia kushuhudia michezo mbalimbali mjini London.

Kemboi, ambae ni bingwa wa mwaka 2004. ametetea ubingwa wake baada ya mwanaridaha mwengine wa Kenya, Brimin Kipruto, kuachwa nyuma raundi moja kabla ya kumalizika mchuano huo ambapo alishinda kwa dakika nane na sekunde chache.

Mkimbiaji mwingine Mfaransa, Mahiedine Mekhassi, ambae ni rafiki wa karibu wa Kiomboi aliibuka na medali ya fedha, na Mkenya Abel Mutai alishinda medali ya shaba.

Kipruto ambae alianguka baada ya kuonekana kama ameteguka mguu alimaliza kwa kushika nafasi ya tano. Kiomboi, ambae amekuwa bingwa wa dunia mara mbili, alionekana katika pembezoni mwa uwanja akipunga mkono kama ishara ya kushangilia ushindi wake.

Bwana huyo anaibuka kidedea huku akikabiliwa na tuhuma za kumchoma kisu mwanamke mmoja nchini Kenya, tukio lililotokea Juni, ambalo mpaka sasa sakata hilo halijamalizika. Mkimbiaji huyo ambae ni afisa wa polisi alikanusha mashitaka yanayomkabili, na Kamati ya Olimpiki ya Kenya ilimsafisha mwaanriadha huyo mwenye umri wa miaka 30 ili aweze kushiriki mashindano haya ya London kwa kusema kwa sasa ni mtu msafi mpaka pale atakapokutwa na hatia.

Ama kwa upande mwingine, Usain Bolt kutoka Jamaica aliwanyamazisha baadhi ya mashabiki wa mchezo huo baada ya kuibuka kifua mbele katika mbio za mita 100, ikiwa ni kama kumpigia mstari kabisa ile nafasi yake ya kuwa mwanariadha mwenye kasi kubwa kabisa kuliko yeyote duniani.

Katika kinyanganyiro cha jana, mwenzake Yohan Blake alinyakua medali ya shaba. Ushindi huo ulipatikana siku mbili kabla ya Taifa la Jamaica kusheherekea miaka 50 ya uhuru wake baada ya utawala wa Uingereza.

Baadhi ya watu waliweka alama za kujiuilza vichwani kama kweli Bolt ataweza kufurukuta katika mchuano huo, hasa baada ya kukabiliwa na maumivu ya mgongo.

Katika hatua nyingine katika hali iliyowashangaza wengi, polisi sasa inamshikilia shabiki mmoja alietupa chupa uwanjani kabla ya kuanza kwa mbio za mita 100. Msemaji wa Polisi nchini Uingereza anasema shabiki huyo alianza kupaaza sauti na kutoa maneno makali kabla ya kufanya kitendo hicho.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Miraji Othman