1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi maarufu Zanzibar,Ali Mohamed Nabwa amefariki dunia

15 Februari 2007

Mwandishi habari maarufu Zanzibar, Ali Mohammed Ali Nabwa, aliyewahi kunyang'anywa uraia baada ya kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, kabla ya kurudishiwa hivi karibuni, amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo katika hospital ya Muhimbili,Dar es Salaam. Mazishi yake yamefanyika kisiwani Zanzibar.

https://p.dw.com/p/CHK3
Mwandishi wetu wa Zanzibar, Salim Said Salim aliyekuwa akijuana na marehemu kwa zaidi ya miaka arobaini na kufanya kazi naye katika vyombo tofauti vya habari anaeleza zaidi juu ya maisha yake.