1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwishoni mwa wiki

Ramadhan Ali12 Oktoba 2007

Firimbi inalia Afrika kwa Kombe la dunia 2010,nusu-finali ya kombe la rugby kati ya Uingereza na Ufaransa na Argentina na afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/C7nQ

Tukianza na Bundesliga,ligi ya Ujerumani,viongozi wa Ligi Bayern Munich waliofungua mwanya wa hadi pointi 5 jumamosi iliopita wanaumana wakati huu dakika za mwisho na Bochum wakati mahasimu wao wa karibu Bremen wanacheza na Hertha Berlin.Mabingwa Stuttgart wanatolewa jasho na hamburg wakati Bayer Leverkusen iliopo nafasi za juu kileleni iko nyumbani ikipambana na Borussia Dortmund.

Nuremberg wanatmba wakati huu nyumbani na Frankfurt.Schalke ilikomewa mabao 2:0 jumamosi iliopita na chipukizi karlsruhe inaumana na Hansa Rostock kutoka mashariki mwa Ujerumani.

Kesho jumapili mapambano 2 yanakamilisha dibaji ya mwishoni mwa wiki hii: hannover ina miadi na Wolfsburg wakati Karlsruhe inakutana na Bielefeld.

Barani Afrika firimbi kesho Italia kuanzisha kinyan’ganyiro cha kuania tikiti 5 za Afrika kwa kombe la dunia la kwanza barani humo 2010 nchini Afrika Kusini.kwavile, hakuna nchi ya kiafrika inayotaka kukaa kando ya Afrika Kusini likianza kombe la dunia,majirani 2 Comoro na Madagascar wanaanza kesho kuania tikiti zao.

Madagascar lakini ina kibarua kigumu kufuta madhambi yake ya siku za nyuma inapokutana na visiwa vya Ngazija.

Kwa Comoro, hii ni historia.Kwani, itakua mara ya kwanza kabisa Comoro inashiriki katika kuania tiketi ya Kombe la dunia.Comoro imecheza mechi 3 tu za kimataifa tangu kujiunga na FIFA miaka 2 iliopita.

Mjerumani Franz Gerber ndie kocha wa Madagascar nae amewaingiza washambulizi 2 kutoka klabu za reunion-nao ni akina Patrick Bruhto na Pamphile Rabefitia.

Mpambano wa marudio utachezwa mjini Moroni hapo nov.17 na hiyo itakua mara ya kwanza kwa mapambano ya kimataifa kuchezwa visiwani humo.

Mpambano wa kesho jumapili ni mmoja kati ya mapam,bano 3 ya duru za kwanza kabla kura ya timu za kombe la dunia zitakavyoumana kupigwa mjini Durban,Afrika Kusini hapo Nov.25.

Hapo Oktoba 17,Sierra Leone itaikaribisha Guinea Bissau mjini Freetown huku duru yapili kati yao imepangwa Nov.17 huko Bissau.Djibouti itacheza na jirani yake Somalia huko Djibouti hapo nov.17.

Ama katika kandaya Amerika kusini kesho Brazil inakaribishwa nyumbani na Colombia wakati Paraguay inaitembelea Peru katika duru za kwanza za kanda yao kuania tiketi za kwenda Afrika kusini 2010.

Rais wa FIFA Sepp Blatter amethibitisha mwishoni mwa wiki hii kwamba anataka kuuzika mtindo wa zamu wa kuandaa kombe la dunia kutoka bara moja hadi jengine.hii itaifungulia mlango Uingereza kugombea kuandaa kombe hilo 2018 baada ya kuwa mwenyeji 1966.

Blatter aliambia Idhaa ya BBC kati ya wiki hii kuwa anaona kuna sababu za kubadili mfumo wa sasa baada ya Colombia na Argentina kujitoa katika kinyan’ganyiro cha kuania kuandaa kombe la dunia 2014 na hivyo kuachia Brazil kuwa mgombea pekee.Brazil iliandaa kombe la dunia 1950.

Ujerumani iliandaa kombe hili la dunia mwaka jana 2006 na Afrika kusini zamu yake 2010 na halafu itafuata Brazil 2014.

Rais wa FIFA amesema hatahivyo, ataungamkono kwa bara lolote kuandaa kombe la dunia ikiwa hakuna nchi ya bara hilo ilioandaa mojawapo ya mashindano 2 yaliopita.

RUGBY:

Kesho asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano uwanjani Stade de France, mjini Paris,Ufaransa.Baada ya nusu-finali ya kwanza leo kati ya wenyeji Ufaransa na Uingereza,mabingwa watetezi, kesho ni zamu ya puma wa Argentina kutafunana na Springboks-Afrika Kusini kwa nusu-finali ya pili.

Afrika Kusini ni mabingwa wa 1995 na wanataka kesho kukata tiketi nyengine ya finali na kurudi na kombe hilo Johannesberg,ili kuandaa kombe la dunia la FIFA 2010.

Tayari kampuni la umeme la Afrika Kusini (ESKOM) limewataka wateja wake kupunguza matumizi ya umeme ili kuepusha kujakatiwa umeme wakati wa nusu-finali ya kesho.

Springboks wanasema azma yao kesho ni kuwatia adabu puma wa Argentina waliotamba hadi sasa na kufululiza hadi nusu-finali yao ya kwanza kabisa.1999 Puma walifika robo-finali, lakini mara hii wametia for a hadi nusu-finali wakiziacha nyuma mabingwa mara kadhaa New Zealand-all-blacks na hata Kangaruh –Australia.

Hatahivyo, Springboks wanajua hawatateremka mlima.Kuwasili nusu-finali ya kesho,springboks waliwatoa kwa taabu sana FIJI kwamabao 37-26.Argentina wamewapiga kumbo waskochi-Scotland.

Kwa changamoto ya kesho,Argentina imeteua kikosi kile kile kilichocheza na Scotland.Nahodha wao Pichot,amejiwinda kuiongoza jahazi yake hadi bandarini-finali.

Afrika Kusini kwa upande wake inajaribu kuwasili finali kwa mara ya pili na kulirejesha nyumbani Kombe walilolitwaa 1995 mbele yam zee Nelson Mandela.

Puma wa Argentina kwa upande wao watajaribu kesho kuwalaza springboks kwa mara ya kwanza baada ya kulazwa mara zote 11 na springboks walizokutana.Mpambano wao wa awali kabisa ulikuwa 1993.

Kwahivyo, iliobaki sasa tusiandike mate na wino upo-tusubiri changamoto hapo kesho.