1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwito kuidhinisha Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CazO

BERLIN:

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel ametoa mwito kwa bunge la Ujerumani,kuidhinisha haraka Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya utakaotiwa saini leo hii mjini Lisbon,Ureno.Alipohotubia bunge la Ujerumani-Bundestag mjini Berlin Merkel alisema, ni matumaini yake kuwa mkataba huo utaidhinishwa hadi ifikapo mwezi Mei mwaka 2008.

Merkel amesema,hatimae kufanikiwa kupata Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya,ni hatua iliyo na umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa Ulaya.

Akaongezea kuwa kuambatana na mfumo mpya wa upigaji kura,demokrasia itazidi kuimarishwa katika Umoja wa Ulaya.Ni matumaini yake kuwa nchi zingine pia zitaidhinisha mkataba huo mpya,ili upate kufanya kazi kuanzia mwaka 2009. Mkataba huo utachukua nafasi ya katiba iliyopendekezwa hapo awali na kukataliwa na wapiga kura nchini Ufaransa na Uholanzi miaka miwili iliyopita.