1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwito kusaidia mchakato wa amani Mashariki ya Kati

24 Septemba 2010

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa mwito kwa viongozi wa kimataifa kusaidia jitahada za kutafuta suluhisho la amani kumaliza mgogoro kati ya Waisraeli na Wapalestina.

https://p.dw.com/p/PLRc
U.S. President Barack Obama addresses the 65th session of the United Nations General Assembly on Thursday, Sept. 23, 2010 at United Nations headquarters. (AP Photo/Richard Drew)
Rais wa marekani, Barack Obama akihotubia kikao cha 65 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.Picha: AP

Katika hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Obama alisema kuwa ni muhimu kwa pande zote kushirikiana ili katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, kuweze kupatikana taifa huru la Palestina na Israel inayoweza kuishi kwa usalama.

Akifafanua alisema kuwa Waisrael na Wapalestina wanapaswa kuleta amani, lakini kila mmoja wetu anawajibika pia kutoa mchango wake.

Mahmoud Ahmadinejad, President of Iran, holds up a copies of the Quran, left, and Bible, right, as he addresses the 65th session of the United Nations General Assembly at U.N. headquarters Thursday, Sept. 23, 2010. (AP Photo/Richard Drew)
Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad akihotubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mikononi mwake ameshika Quran na Biblia.Picha: ap

Baadae Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran alihotubia baraza hilo. Lakini dakika chache baadae wajumbe wa Marekani walitoka kwenye ukumbi huo,wakifuatwa na wajumbe wengine wa nchi za Ulaya ya Magharibi.

Ahmedinejad alizungumzia juu ya nadharia kuwa serikali ya Marekani ndio iliyohusika na shambulio la Septemba 11 ili iweze kujiimarisha zaidi katika Mashariki ya Kati pamoja na kuimarisha uchumi wake.

Hapo awali Rais Obama alieleza waziwazi kuwa ataendelea kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo unaohusika na mradi wa nyuklia wa Iran. Lakini serikali ya Iran mjini Tehran yapaswa kuthibitisha kuwa mradi huo ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu.