Mzozo baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda
22 Juni 2012Matangazo
Siku mbili baada ya raia 11 wa Rwanda kukamatwa mjini Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kupigwa vibaya kisha kuvukishwa mpaka kwa nguvu hadi Rwanda, nchi hiyo imeionya kwa barua Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Rwanda Bi Louise Mushikiwabo amesema kuendelea kuitaja Rwanda kama chanzo cha tatizo la DRC ni hatari kwa raia wake na raia wenye asili ya Rwanda waishio DRC.
Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.
(Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Sylvanus Karemera
Mhariri: Josephat Charo