1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa gesi kati ya Russia na Belorussia

9 Januari 2007

Mzozo wa gesi kati ya Moscow na Minsk watishia kuathiri Ulaya magharibi.Mshikamano na mwenyekiti wa CSU Bw.Stoiber ni mada nyengine iliochambuliwa leo na wahariri.

https://p.dw.com/p/CHU1

Kwanza kuzuwia Russia shehemu ya shehena yake ya gesi kuja Ulaya kutokana na mvutano wake na Belorussia na mada ya pili, mshikamano uliooneshwa na vigogo vya chama cha CSU huko Bavaria kwa kiongozi wa chama na waziri-mkuu Edmund Stoiber:

Gazeti la Kölner Stadt-Anzeiger linachambua athari za kisiasa za hatua ya Russia ya kuzuwia kwa sehemu gesi yake kuchururika Ulaya.Laandika:

Mvutano wa hivi sasa wa Russia na jirani yake Belorrusia una pia sababu za kisiasa.Russia imevunjika moyo kumuona dikteta wa Belorussia,rais Lukaschenko amerudi nyuma kutekeleza ule muungano wa nchi hizo mbili uliotapiwa miaka mingi nyuma….Shinikizo la sasa kali la kiuchumi, pengine laweza sasa kufanya kazi kutimiza shabaha hiyo.

Rais Putin huenda hapo akavuna matunda mema,kwani,kwa Russia kujitanua zaidi mipaka yake hadi Belorussia,kunaweza kukamfungulia mlango wa kuchaguliwa tena 2008 na hivyo kutobidi kun’gatuka.”-ni maoni ya Kölner Stadt-Anzeiger.

Ama gazeti la FINANCIAL TIMES la Ujerumani linahisi kuwa Russia kuanzia miezi iliopita imekuwa hatua kwa hatua ikimshinikiza jirani yake huyo.

Katika UU,ambao usuhuba wake na Belorussia umebakishwa katika maswali muhimu tu,unaweza kuridhikka na hali hii.Kwani, dikteta huyo ananyimwa pumzi za kuvuta.Hatahivyo, kitendo hiki cha Russia, kinabainisha tena jinsi gani Kremlin isivyojali mradi tu inasukuma mbele siasa zake za nje na masilahi yake ya kiuchumi.

Katika neema ya sasa kwenye soko la mafuta na gesi,uongozi wa Russia unaonesha jeuri inayomfanya mtu kuiogopa- FINANCIAL TIMES Deutschland.

Gazeti la jiji hili la Bonn-Bonner General Anzeiger, linajishughulisha na kutegemea Ujerumani mafuta ya Urusi:

Linasema kuwa, endapo viongozi wenye usemi huko Moscow au Minsk wakifunga bomba la mafuta, basi watu waweza kuanza kujikunja kwa baridi nchini Ujerumani.

Kumiliki nishati hii leo, ni kumiliki nguvu.Kusema wazi zaidi, ni hivi-nishati nchini Ujerumani inategemea nia njema ya viongozi wa Kremlin.Kutegemea tu mafuta ya nchi za kiarabu ni tayari hatari ya kutosha……

Gazeti la OSTTHÜRINGERZEITUNG kutoka Gera,linaona wanasiasa hapa wamepewa changamoto:

Laandika kuwa, siasa ya nje ya Ujerumani daima ikishiklamana na sera ya nishati.Ni muhimu kwa Ujerumani kuwa na uhakika wa kujipatia mali ghafi hiyo muhimu sana .Na nchini wanasiasa wanapaswa kufanya kila wawezalo ,kuachana na kutegemea mno mafuta na gesi na hivyo kusaka na kukuza nishati za aina nyengine-ni nasaha ya OSTTHÜRINGER ZEITUNG.

Likitubadilishia mada, gazeti la AUGSBUGER ALLGEMEINE linazungumzia mshikamano wa vigogo vya chama cha CSU huko Bavaria, kwa mwenyekiti na waziri-mkuu wao kuwa hata mwakani 2008 ndie mtetezi wao mkuu kwenye uchaguzi wa mkoa huo.Laandika:

“Kwa sasa, Bw.Edmund Stoiber amevuta pumzi.

Chama kimempa muda wa kijirekebisha mwenyekiti huyo aliewapatia ushindi mkuu katika uchaguzi uliopita.Kimefanya hivyo hata kwa hatari ya kuukosea wakati muwafaka wa kumbadili kiongozi wake.Mwaka huu Bw.Stoiber atabidi hatahivyo, kukiyakinisha chama kwamba aweza tena kukiongoza katika ushindi mwaka ujao.La sihivyo, chama cha CSU, kitajionea balaa lisilo kwisha na pengine mwisho wenye balaa .