1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NÜRENBERG: Idadi ya wakosa ajira yapunguka Ujerumani

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCo1

Tarakimu rasmi zilizotangazwa hii leo zinaonyesha kuwa idadi ya watu wasio na ajira imepunguka katika mwezi wa Novemba na ni chini ya milioni nne.Matokeo ya uchumi unaoendelea kustawi nchini Ujerumani,yanadhihirika katika soko la ajira.Kwa mujibu wa ofisi kuu ya ajira ya Ujerumani mjini Nürenberg,katika mwezi wa Novemba idadi ya wakosa ajira imepunguka hadi asili mia 9.6 kulinganishwa na asilimia 9.8 mwezi mmoja uliopita.Vile vile ni mara ya kwanza tangu Oktoba mwaka 2002 kwa idadi ya watu waliokosa ajira kuwa chini ya milioni nne.