1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NÜRNBERG: Idadi ya wakosa ajira yapunguka mwezi Machi

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEP

Kwa mara nyingine tena nchini Ujerumani,idadi ya watu wanaotafuta ajira imepunguka mwezi huu, kulinganishwa na mwezi uliopita.Takwimu zilizotolewa na Shirika la Ajira la Ujerumani mjini Nürnberg huonyesha kuwa katika mwezi wa Machi watu milioni 4.1 wamekosa ajira. Kulinganishwa na mwezi uliopita,hiyo ni kama watu 114,000 wachache.Kwa hivyo idadi ya watu wasio na ajira imeangukia asilimia 9.8 kutoka asilimia 10.1 hapo mwezi Februari.