1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABLUS: Israel imemuua kiongozi wa Islamic Jihad

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcf

Wanajeshi wa Kiisraeli wamempiga risasi na kumuuwa kiongozi mmojawapo wa kundi la Islamic Jihad katika mji wa Nablus,ulio kwenye Ukingo wa Magharibi.Kwa mujibu wa duru za usalama za Kipalestina,Raed Abu Al Adfas aliekuwa na miaka 26,alikutikana amekufa baada ya kuzuka mapambano ya kufyatuliana risasi na wanajeshi wa Kiisraeli. Duru hizo zikaongezea kuwa mwanachama mwengine wa Islamic Jihad alikamatwa na vile vile mpita njia mmoja alijeruhiwa katika mapambano hayo.