1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nablus: Majeshi ya Israel yaingia tena katika mji wa Wapalastina wa Nablus

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNs

Majeshi ya Israel yameuvamia tena mji wa Nablus ulioko Magharibi ya Mto Jordan, ikiwa ni siku moja baada ya kuondoka kutoka eneo hilo ambalo ni ngome ya Wapalastina wenye siasa kali. Magari kadhaa, yakisaidiwa na makarandinga, yaliingia Nablus alfajiri ya leo, na barabara zinazotokea mji huo zilifungwa. Washukiwa watano walikamatwa katika msako wa nyumba hadi nyumba kuwatafuta wapiganaji wa Kipalastina. Msako mkali katika mji huo ulianza jumapili iliopita. Jeshi la Israel limesema operesheni hiyo imekuwa ya lazima kwa vile wengi wa watu wanaojiripouwa kwa kujitolea mhanga wanaojaribu na kuingia Israel kutoka Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wanatokea Nablus.

Kwa upande mwengine, majeshi ya usalama ya Kipalastina katika mji wa Jenin ulioko katika Ukingo wa Magharibi yanasema majeshi ya Israel yamewauwa Wapalastina watatu wa kikundi cha Kiiislamu cha Jihad wakati wa msako wa nyumba hadi nyumba.