1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABLUS: Vifaru vya Israel vimeingia mji wa Wapalestina

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOf

Wanajeshi wa Kiisraeli wakiwa katika vifaru na magari ya kijeshi wameingia mji wa Wapalestina wa Nablus ulio katika Ukingo wa Magharibi na wakazi wameamriwa kutotoka majumbani mwao.Kwa mujibu wa jeshi la Israel,hatua hiyo imechukuliwa baada ya kugundua maabara ya miripuko katika mji huo na polisi kufyatuliwa risasi katika sehemu mbali mbali za mji.