1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABLUS: Wapalestina wameamriwa kubakia majumbani mwao

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOX

Vifaru na magari ya kijeshi ya Israel yameuvamia mji wa Nablus katika Ukingo wa Magharibi na maelfu ya Wapalestina wamepewa amri ya kutotoka majumbani mwao na hata barabara zimezibwa.Kwa mujibu wa jeshi la Israel si chini ya watu 30 wamekamatwa na akwamba hatua hiyo imechukuliwa baada ya maabara ya miripuko kugunduliwa katika mji wa Nablus siku ya Jumamosi.Wakati huo huo redio ya Israel imeripoti kuwa wanajeshi 2 wa Kiisraeli,walijeruhiwa katika mripuko mmoja.