1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAHR AL-BARED:Jamii za wapiganaji wa kiislamu waondoka

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWP

Jamii za wapiganaji wa kiislamu wanaopambana na jeshi la Lebanon wanaanza kuondoka kambi ya wakimbizi wa Palestina iliyo kaskazini mwa Lebanon.Kambi hiyo imekuwa ikizongwa na ghasia kwa muda wa miezi mitatu iliyopita baada ya jeshi la nchi kuwashambulia wapiganaji wa kiislamu.

Kwa mujibu wa wakazi walioshuhudia jeshi la Lebanon liliagiza waandishi wa habari kutofika mahala hapo ambapo wakazi wake wakiwemo wanawake 22 na watoto 41 wanaondoka.