1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAHR AL BARED:Jeshi lashambulia tena kambi ya wakimbizi

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjU

Jeshi la Lebanon limeanza tena kushambulia kambi ya wakimbizi ya Nahr al Bared ili kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Fatah al Islam wanaoaminika kuhusika na kundi la Al Qaeda.Wapiganaji hao wanajificha katika kambi hiyo tangu katikati ya mwezi wa Mei.

Wanajeshi wawili wanaripotiwa kuawa huku mapigano makali yakiendelea.Idadi kamili ya watu waliokufa mpaka sasa imefikia 176 wakiwemo wanajeshi 88 na yapata wapiganaji 68 tangu mapigano kuanza .

Mapigano hayo mapya yanatokea ikiwa ni siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya kwanza tangu vita kutoa kati ya Israel na wanamgambo wa Kishia wa Hezbollah.Vita hivyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1200 nchini Lebanon pekee.

Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora anatoa wito kwa jeshi la nchi hiyo kuwafurusha wapiganaji wa Fatah al Islam.