1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAHR AL-BARED:Mapigano mapya Beirut

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvx

Mapigano yamezuka tena hii leo kati ya majeshi ya serikali yanayoshika doria kwenye kambi moja ya wakimbizi wa Kipalestina na wapiganaji wa kiislamu.Ghasia hizo zimeingia siku yake ya 13 katika eneo la kaskazini mwa Lebanon.Hakuna taarifa zozote za majeruhi zilizotolewa kwenye kambi hiyo ya Nahr el Bahred iliyo karibu na mji mkuu wa Beirut.

Kulingana na duru za jeshi mwanajeshi mmoja aliuawa hapo jana nao wapiganaji 8 wa kiislamu walipoteza maisha yao katika mapigano makali ya juzi.Mapigano hayo yalisababisha wanajeshi wawili kujeruhiwa.Watu 80 mpaka sasa wamepoteza maisha yao katika ghasia hizo wakiwemo wanajeshi 35 tangu mapigano kuanza katikati ya mwezi uliopita.

Serikali ya Lebanon kwa upande wake inashikilia kuwa kundi hilo la wapiganaji la Fatah al Islam liwafikishe wapiganaji wake kuhukumiwa baada ya kuhusika katika mashambulizi ya mwaka 75 hadi 90 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Fatah al Islam wanasisitiza kuwa hakuna mpiganaji wao yoyote atakayehukumiwa.

Zaidi ya thuluthi mbili ya wakazi wa Nahr al Bared wameachwa bila makao kwasababu ya mapigano hayo.Mashirika ya misaa yanatia juhudi kusambaza misaada kwa walioweza kukimbia au waliosalia kambini.

Baraza la Usalaama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuundwa kwa mahakama maalum kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya marehemu Waziri mkuu Rafiq Hariri yaliyotokea mwaka 2005 katika shambulio la bomu.Nchi jirani ya Syria inalaumiwa kutekeleza mauaji ya kiongozi huyo wa zamani na mengine.Syria kwa upande wake inashukilia kuwa haijahusika na kushikilia kuwa haitashirikiana na mahakama hiyo mpya.