1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAHR EL-BARED:Siniora asema jeshi lake limeushinda ugaidi

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBT9

Takriba wapiganaji wenye masimamo mkali 39 wameuwawa katika mapigano na jeshi la Lebanon kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr El-Bared.

Jeshi la Lebanon pia limewapoteza askari wake watatu katika mapigano hayo, wapiganaji wenye msimamo mkali 20 wamekamatwa.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora amesema juhudi za majeshi yake za kuidhibiti tena kambi hiyo ya wakimbizi wa Kipalestina kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Fatah al Islam ni ushindi mkubwa dhidi ya ugaidi.

Amesema serikali yake itaijenga tena upya kambi hiyo.

Zaidi wa wakimbizi elfu 40 waliokuwa wakiishi kwenye kambi hiyo walitoroka mara tu mapigano yalipozuka mapema mwezi Mei.