1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Afrika lazima ioane na mabadiliko ya hewa

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvl

Nchi za Kiafrika lazima zijirekebishe kuweza kuhimili athari za kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani ili kuzuwiya taathira zaidi ambayo mabadiliko ya hali ya hewa inaweza kusababisha kwa watu wake zaidi ya milioni 800.

Kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara halina budi kuboresha mifumo yake ya hivi sasa ya kuchunguza hali ya hewa na kufungamanisha kwa karibu zaidi utafiti wa mazingira na sera za serikali.

Maafisa wa serikali,wanasayansi na wanaharakati takriban 6,000 kutoka duniani kote wanatazamiwa kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Hali Hewa unaofunguliwa mjini Nairobi Kenya hapo kesho ambacho ni kikao cha kwanza juu ya mabadiliko ya tabia nchi kuwahi kufanyika kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.