1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Bunge laaza kikao.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCH0

Bunge la Kenya limeanza kikao kipya jana , lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa wanasiasa watakuwa katika harakati za kuwania kuchaguliwa tena kabla ya uchaguzi mwaka huu na kuacha kushughulikia masuala muhimu bungeni.

Uchaguzi wa bunge na rais unatarajiwa kwa kiasi kikubwa kufanyika katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa katika Afrika mashariki mwezi wa Desemba.

Rais Mwai Kibaki ambaye serikali yake ya mseto iliingia madarakani mwaka 2002 kwa ushindi wa kishindo, ameonyesha nia ya kutaka kugombea kipindi cha pili, licha ya kuwa bado hajatangaza rasmi nia yake hiyo.

Miezi tisa kabla ya uchaguzi huo , magazeti tayari yamejaa taarifa juu ya uwezekano wa ushirika na makubaliano ya kisiasa baina ya viongozi wa upinzani katika kuelekea uchaguzi wa nne wa kidemokrasia tangu nchi hiyo kupata uhuru kutoka Uingereza 1963.