1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Ethiopia yahofia vita kuzuka kati yake na Eritrea.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1J

Ethiopia imetoa wito jana kwa umoja wa mataifa kumpeleka mjumbe mpya kusaidia kutatua mzozo wa muda mrefu wa mpaka na jirani yake Eritrea mzozo ambao unatishia kufikia katika hatua ya vita katika wiki za hivi karibuni.

Taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni ya Ethiopia imesema kuwa nchi hiyo inaamini kuwa kuna haja ya kuwa na mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kuongeza juhudi zake katika suala hilo. Imeongeza taarifa hiyo kuwa Ethiopia itaunga mkono juhudi hizo. Taarifa hiyo inakuja siku moja baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuyataka mataifa hayo mawili ya pembe ya Afrika kutatua tatizo lao la mpaka kwa amani na kuchukua hatua sahihi za kuweka alama katika mpaka wao.