1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Ghasia zazuka katika uchaguzi.

17 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImL

Ghasia zimechafua kampeni za mwanzo za uchaguzi wa bunge jana Ijumaa nchini Kenya , kabla ya kile kinachotarajiwa kuwa uchaguzi ambao utakuwa na mvutano mkubwa mwezi ujao. Wafuasi wa wagombea hasimu waliokuwa na hasira walipambana karibu katika majimbo yote manane ya nchi hiyo wakati majeshi ya usalama yakihangaika kurejesha amani. Ghasia hizo zilizuka wakati vituo vya kupigia kura vilipofunguliwa kwa ajili ya uchaguzi wa wagombea wa vyama , kwa ajili ya uchaguzi wa hapo desemba 27 wa bunge. Uchaguzi wa rais pia utafanyika siku hiyo hiyo. Wagombea waliombele katika uchaguzi wa rais walitoa wito wa utulivu wakati tume ya uchaguzi ikiidhinisha wagombea tisa wa kiti cha urais.