1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Kenya yaonya wanaofikiria kuishambulia.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5K

Maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la ulinzi nchini Kenya wameonya jana kuwa yeyote atakayejaribu kuigusa Kenya atakabiliwa na nguvu za jeshi la nchi hiyo, siku moja baada ya wanamgambo wa Kisomali kujisogeza kwenye kijiji cha mpakani na Kenya na kisha baadaye kuondoka.

Waziri wa nchi anayehusika na ulinzi nchini Kenya Njenga Karume amekataa kutaka kundi ama watu na kusema kuwa Kenya haioni haja ya kuweka majeshi yake mpakani na Somalia kwa sasa , licha ya kwamba imeongeza doria ya polisi.

Mjini Geneva , shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi limesema jana kuwa idadi ya Wasomali wanaokimbilia nchini Kenya imeongezeka mno na inaweza kuathiri uwezo wa mashirika ya kutoa misaada.