1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Kiongozi wa zamani wa waasi nchi Uganda, Alice Lakwena, afariki dunia.

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZw
Rais Vladimir Putin akiwa katika mavazi ya kijeshi.
Rais Vladimir Putin akiwa katika mavazi ya kijeshi.Picha: AP

Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Uganda, Bibi Alice Lakwena amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Polisi wa Kenya, Alice Lakwena alifariki mkesha wa kuamkia leo katika kambi ya wakimbizi ya Daadab takriban kilomita mia sita kaskazini mashariki mwa Nairobi.

Bibi Alice Lakwena alikuwa amejitangaza kuwa nabii na akaongoza vita kwa nia ya kumpindua Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Vikosi vya Alice Lakwena vilishindwa mwaka 1987 na akakimbilia nchíni Kenya.

Baadhi ya wafuasi wake waliunda kundi jipya la Lords Resistance army lililoongozwa na mpwa wake, Joseph Kony.