1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Mahakama yaamuru uchunguzi mpya.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBd6

Mahakama moja nchini Kenya imeamua kuwa kifo cha kutatanisha cha mchungaji wa Kimarekani mwaka 2000 kilikuwa ni mauaji na kuamuru polisi kufanya upya uchunguzi.

Jaji ya mahakama mjini Nairobi Maureen Odero amesema kuwa mchungaji John Anthony kaiser , ambaye mwili wake ulikutikana na majeraha kadha ya risasi kando ya barabara katika eneo la kati nchini Kenya la Rift Valley August 24, 2000 kuwa aliuwawa.

Tetesi zilizagaa nchini Kenya kuwa mchungaji Kaiser ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi, alikuwa mhanga wa kazi iliyofanywa na serikali.

Wataalamu wa alama za ushahidi kutoka katika kitengo cha FBI nchini Marekani walieleza mwaka jana baaya kifo cha mchungaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 67 kuwa huenda alijiua.