1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mawaziri wa ulinzi wajadili kuundwa kikosi cha usalama

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYM

Mawaziri wa ulinzi wa nchi za Afrika Mashariki wamekutana leo mjini Nairobi Kenya kujadili kikosi cha kanda hiyo kwa ajili ya kikosi cha Umoja wa Afrika kilichoundwa mnamo mwaka 2004.

Licha ya kikosi hicho kuanzishwa rasmi wakati huo, mpaka sasa bado hakijaanza kufanya kazi kutokana na upungufu wa fedha.

Makamanda wa jeshi kutoka nchi 13 wamejadili kikosi cha Afrika Mashariki kitakachokuwa na wanajeshi 3,000. Kikosi hicho kitakuwa na kazi ya kukabiliana na mizozo ya kivita na majanga asili.

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, ameliambia baraza la mawaziri wa ulinzi na usalama wa eneo la Afrika Mashariki wafanye haraka kukamilisha kikosi hicho kinachohitajika kwa dharura.

Aidha rais Kibaki amewatolea mwito wahisani wasaidie kutoa dola milioni 2.5 kwa ajili ya kikosi hicho.