1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mazungumzo juu ya rasimu mpya ya kupunguza gesi zinazochafua hewa kuanza mwaka 2008

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrn

Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa uliokuwa ukifanyika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, umekamilisha shughuli zake kwa kuamua kuanza mazungumzo mwaka wa 2008 kwa lengo la kupunguza gesi mbaya aina ya dioksidi ya kaboni kabla ya kufikia mwaka 2012. Hapo ndipo rasimu ya Kyoto itamaliza muda wake. Maofisa kwenye mkutano huo wa mjini Nairobi, wamesema Uchina na India ambazo kiwango cha utoaji gesi inayoyachafua mazingira kimezidi kupanda, zimekataa kujiunga mapema na mazungumzo ya kupunguza gesi hiyo. Mashirika ya kuhifadhi mazingira ya Greenpeace na Friends of Earth, yamelalamika kuhusu uchovu uliogubika mkutano huo wa mjini Nairobi, yakidai kuwa mipango ya Umoja wa mataifa na Umoja wa Ulaya ya kutoa fidia kwa wahanga wa mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi masikini haitoshi. Waziri wa Ujerumani wa mazingira, Sigmar Gabriel, amesema viongozi duniani, wakiwemo wale wa nchi 8 tajiri zaidi duniani, wangepaswa kutilia kipaumbele swala hilo.

Indoneshia imependekeza kuwa mwenyeji wa mkutano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa mwaka ujao.