1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mkutano wa kupatanisha makundi ya Somalia

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtR

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa amesema,ana matumaini kuwa mkutano wa upatanisho wa Somalia utafanywa katika mji mkuu Mogadishu, lakini tarehe ya 14 Juni huenda ikabadilishwa. Lynn Pascoe alitamka hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi baada ya kurejea kutoka Mogadishu,ambako alikutana na Rais Abdullahi Yusuf Ahmed na Waziri Mkuu Ali Mohamed Gedi wa Somalia.Vile vile alikutana na Ali Mahdi ambae ni rais wa kamati inayotayarisha mkutano huo wa upatanisho.