1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Mwanadiplomasia wa Marekani akutana na spika wa bunge la Somalia

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcY

Mwandiplomasia mwandamizi wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Jendayi Frazer amekuwa na mazungumzo na spika wa bunge la Somalia mjini Nairobi leo hii ambaye amekanwa na serikali ya mpito ya nchi hiyo kutokana na kuwa na mawasiliano na Uongozi wa Kiislam nchini Somalia.

Frazer alikutana na Sharif Hassan Sheikh Aden kwenye hoteli katika mji mkuu huo wa Kenya baada ya kufuta ziara yake mjini Mogadishu kutokana na hali mbaya ya usalama kufuatia kushindwa kijeshi kwa Muunganao wa Mahkama za Kiislam.

Aden mwanasiasa mashuhuri nchini Somalia aliachwa kuungwa mkono na serikali ya mpito ya Somalia hapo mwezi wa Novemba wakati ilipomshutumu kwa kuchukuwa hatua bila ya idhini yake katika kujaribu kuzungumzia suala la amani na Uongozi wa Kiislam ambao ulitimuliwa kwenye miji ya Somalia baada ya vikosi vya Ethiopia kuingia vitani dhidi yao hapo Desemba 20.

Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa juu ya mkutano huo wa Frazer na Aden lakini imeelezwa kwamba mwanadiplomasia huyo wa kike pia anatazamiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa mashirika ya kiraia ya Somalia na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Mohamed Gedi.