1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Nchi masikini zisaidiwe kupambana na madhara ya ujoto duniani

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCry

Ujerumani itazipatia nchi masikini msaada wa teknolojia ya kulinda mazingira.Hayo amesema waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel katika mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa unaofanywa katika mji mkuu wa Kenya,Nairobi.mjini Nairobi.Mkutano huo unashughulikia madhara yanayosababishwa barani Afrika kwa sababu ya ujoto duniani.Baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kutoa mwito kwa nchi tajiri za viwanda kuchukua hatua moja kwa moja,waziri Gabriel alisema,nchi zinazoendelea zipatiwe msaada wa fedha kupambana na matatizo kama vile uharibifu wa misitu. Wanasayansi wanasema nchi zilizo masikini ndio hubeba mzigo wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani,ingawa kipimo cha gesi zinazochafua mazingira katika nchi hizo ni ndogo kabisa.