1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Viongozi wa Kiafrika wasikubali kushinikizwa

8 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C797

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutoka nchi 9 za Kiafrika wamezihimiza serikali zao kutokubali kushinikizwa kutia saini makubaliano mapya ya biashara pamoja na Umoja wa Ulaya hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu.Mwito huo umetolewa kwa mawaziri wao katika hati ya pamoja iliyotiwa saini na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutoka Ghana,Zambia,Zimbabwe,Botswana,Niger,Burkina Faso Nigeria,Afrika Kusini na Kenya.

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya na nchi 78 za Kiafrika na kutoka eneo la Karibea na Pasifiki, zinajadiliana kukamilisha mkataba mpya wa Ushirikiano wa Kiuchumi hadi mwishoni mwa mwaka. Waziri wa Biashara wa Kenya,Mukhisa Kituyi ameutuhumu Umoja wa Ulaya akisema,wakati mfupi uliobakia unatumiwa na umoja huo kwa manufaa yake na kuzishinikiza nchi za Kiafrika.