NAIROBI: Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa waondoka kutoka Somalia
13 Oktoba 2006Matangazo
Umoja wa mataifa umewaondoa wafanyakazi wake kwa muda kutoka Somalia kufuatia vitisho vya kuuawa. Maafisa wa Umoja wa mataifa mjini Nairobi nchini Kenya, hawakusema ni nani ametoa vitisho hivyo lakini wamesema wanavizingatia kwa makini. Wapiganaji wa muungano wa makundi ya waislamu sasa wanalidhibiti eneo la kusini mwa Somalia ukiwemo mji mkuu Mogadishu na serikali ya mpito ya rais Abdullahi Yussufu inaonekana kuwa dhaifu kuweza kudhibiti hali ya mambo Somalia.