1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Watoto 60 walazwa kwa malaria na tumbo la kuhara

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCp2

Takriban watoto 60 wamelazwa kwenye hospitali kuu katika eneo la Kenya ya kaskazini lililokumbwa na mafuriko kufuatia mripuko wa magonjwa ya malaria na tumbo la kuhara.

Watoto hao wamelazwa katika hospitali ya Garissa ilioko kilomta 300 kutoka mji mkuu wa Nairobi baada ya kuripotiwa kuzuka kwa magonjwa hayo kwenye makambi walioko maelfu ya watu waliopoteza makaazi yao kutokana na mafuriko.

Afisa wa afya katika hospitali hiyo Ismael Wango amekaririwa akisema wanaraji kuongezeka kwa idadi hiyo ya wagonjwa.

Mvua mkubwa zilizonyesha kaskazini mwa Kenya zimeuwa takriban watu 80 na kuwapotezea makaazi wengine 200,000.