1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Katibu Mkuu Ban Ki Moon kuweka kipaumbe katika harakati za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Ban Ki Moon ameazimia kuzipa kipaumbele harakati za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa katika muda wake wote wa ukatibu mkuu.

Akizungumza mjini Nairobi kwenye mkutano wa ngazi za juu wa shirika la ulinzi wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, bwana Ki Moon amesema kuwa dunia nzima imo katika hali ya hatari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Katibu Mkuu huyo amelalamika kwamba mzigo mkubwa wa madhara hayo unabebwa na nchi masikini.