1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Meli mbili za Kenya zatekwa Somalia

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1e

Wapiganaji wa Kisomali wameteka meli mbili za uvuvi za Kenya katika pwani ya Somalia kwa mujibu wa afisa mmoja wa ubaharia.Visa vya utekaji wa meli katika eneo hilo vimeongezeka.Meli hizo zilitekwa katika eneo lililo na umbali wa maili 200 kutoka mji wa Mogadishu kulingana na Andrew Mwangura afisa katika Mpango wa Kimataifa wa Mabaharia tawi la Kenya.

Meli hiyo ilikuwa na shehena ya tani alfu 15 ya mizigo iliyotokea Afrika Kusini na kuelekea eneo la Guba.Eneo hilo lililo na urefu wa kilomita 3700 limeshambuliwa sana na watekaji katika kipindi cha mwezi machi mwaka 2005 hadi mwezi Juni mwaka jana.Mashambulio hayo yalikoma wakati Mahakama za kiislamu ziliteka maeneo ya Kusini na katikati ya Somalia.

Majeshi ya Somalia yakiungwa mkono na jeshi la Ethiopia yaliwafurusha wapiganaji wa mahakama hizo mwishoni mwa mwaka jana.Visa vya utekaji vimetokea tena katika kipindi cha majuma machache yaliyopita kwenye eneo ambalo halina usimamizi.