1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Mtu atolewa chupa tumboni

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EY

Madaktari katika mkoa wa kati wametoa chupa ya nusu lita ya bia iliyokuwa imenasa kwenye utumbo mkubwa wa mwanamume mmoja.Mpaka sasa haijulikani namna chupa hioy ilivyoingia tumboni mwake.

Chupa hiyo iliyo na urefu wa inchi 10 ilitolewa mwanzoni mw ajuma hili baada ya kunasa kwenye utumbo mkubwa wa mwanamume mmoja wa umri wa miaka 33.Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya mkoa wa Kiambu. Kulingana na madaktari chupa hiyo haijaathiri viungo vya ndani vya mtu huyo ila huenda alishambuliwa ndipo kitendo hicho cha kustaajabisha kutokea.