1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Muungano wa mahakama za kiislamu bado uko imara

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSj

Afisa wa ngazi ya juu katika muungano wa mahaka za kiislam nchini Somalia, amesema kuwa muungano huo uko imara zaidi hata baada ya kufurushwa na majeshi ya Ethiopea mwaka jana.

Afisa huyo Ibrahim Hussein Adow ambaye anahusika na masuala ya kimataifa katika muungano huo, amesema kuwa wapiganaji wao wako imara ndani ya Somalia.

Akizungumza kutokea Yemen ambako amekimbilia uhamishoni, Adow amesema kuwa wasomali sasa wamejionea wenyewe hali ya usalama duni ilivyo sasa mnamo wakati ambapo nchi hiyo iko chini ya serikali ya mpito inayosaidiwa na Ethiopea.

Amesema kuwa katika kipindi ambacho muungano huo wa mahakama za kiislam ulikuwa ukitawala amani ilikuwa imereja nchini humo..

Marekani na Ethiopea zimekuwa zikiwatuhumu vingozi wa muungano huo mahakama za kiislam kuwa wanamaingiliano na kundi la kigaidi la Al Qaida.