1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Polisi kenya yaua Mungiki 20

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuc

Polisi mjini Nairobi nchini Kenya imewaua watu zaidi ya 20 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi lililopigwa marufuku la Mungiki.

Msemaji wa Polisi nchi humo Eric Kiarathe amesema kuwa watu hao waliuawa wakati wa harakati za jeshi kufuatia kuuawa kwa askari wanne na wanachama wa kundi hilo.

Pia amesema katika msako huo silaha kadhaa zilikamatwa, ambapo baadhi ya askari polisi walijeruhiwa.