1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi.Polisi watawanya waandamanaji.

1 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBdK

Polisi wa Kenya wamewakamata waandamanaji watano na kufyatua mabomu ya gesi ya kutoa machozi walipokuwa wakiwatawanya waandamanaji jana Jumanne waliokuwa wakipinga dhidi ya pendekezo la sheria ya kuwapa mafao ya kiinua mgongo cha dola milioni 20 wabunge wanaomaliza muda wao.

Waandamanaji mamia kadha , ikiwa ni pamoja na baadhi ya wabunge wa zamani, waliimba na kupunga mabango wakati wakiandamana kwenda bungeni wakipinga hatua hizo za kuwapatia wabunge fedha hizo kabla ya bunge jipya kuchaguliwa mwezi Desemba.