1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Rais Kibaki aanza kampeni rasmi

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOu

Rais wa Kenya Mwai Kibaki anaanza kampeni rasmi ikiwa ni siku moja baada ya kutangaza kuwania tena wadhifa wa rais kupitia chama kipya Party of National Unity.Uchaguzi mkuu unapangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa Disemba mwaka huu.Rais Kibaki anaungwa mkono na chama cha KANU ambacho ni mshiriki mkubwa wa muungano huo mpya kilichokuwa madarakani kwa miaka 39 hadi mwaka 2002.

Kulingana na kitengo chake cha habari,wapiga kura sharti wachague wanasiasa wanaoaminika na kuahidi kudumisha usalama katika eneo la Mlima Elgon ambako polisi waliwaua wapiganaji 3 waliokuwa sehemu ya kundi la kikabila linalodai kubatilishwa kwa mpango wa kugawa ardhi.

Zaidi ya watu alfu 66 wameachwa bila makao katiak eneo hilo tangu mwezi Disemba mwaka jana huku wengine 166 kupoteza maisha yao kwa mujibu wa shirika la misaada la Red Cross.

Mwezi jana rais mstaafu Daniel arap Moi aliahidi kumuunga mkono Rais Kibaki kuwania tena nafasi hiyo.