1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Rais wa Kenya awataka wananchi waweke amani kuelekea uchaguzi

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkh

Rais Mwai Kibaki wa Kenya jana amewataka wananchi wake kuweka amani kufuatia kuongezeka kwa ghasia katika taifa hilo linaloeleka kufanya uchaguzi wa bunge na rais mwishoni mwa mwaka.

Rais Kibaki ameapa kutoruhusu wahalifu wowote kwenye nchi yake huku polisi wakizidisha opresheni dhidi ya kundi haramu la Mungiki linalodaiwa kuendesha mauaji nchini humo.

Akitoa hotuba yake kwenye kanisa katoliki hapo jana rais Kibaki alisema serikali yake itatekeleza wajibu wake wa kuwalinda wananchi na mali zao na vile vile itaendelea kuwaadhibu vikali wanaofanya vitendo vya uhalifu.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wanasema kundi la Mungiki linalofungamanishwa na masuala ya kisiasa limeua watu zaidi ya 41 tangu mwezi Marchi hasa kwenye eneo la mji wa Nairobi na eneo la kati mwa Kenya.

Ghasia zimeongezeka katika taifa hilo la Afrika mashariki wakati uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika mwezi Desemba ambapo rais Kibaki anatazamiwa kusimama tena kugombea kiti hicho.