1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi:Serikali yamsajili Biwott kuwa mkuu wa Upinzani

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCob

Serikali nchini Kenya imemsajili Bw Nicholas Biwott kuwa mwenyekiti rasmi wa chama cha upinzani cha KANU. Biwott anachukua wadhifa huo uliokua ukishikiliwa na Uhuru Kenyatta tangu uchaguzi mkuu 2002. Mkutano wa tawi la KANU linaloongozwa na Bw Biwott uliofanyika mjini Mombasa ijumaa iliopita ,uliwaondoa kwenye uongozi Mabwana Kenyatta kama mwenyekiti , Makamu wake Chris Okemo na William Ruto akiwa katibu mkuu , na badala yake kumchagua Bw Biwott kuwa Mwenyekiti na Katana Ngala Makamu mwenyekiti. Hata hivyo katika mkutano wao wa Nairobi hapo jana tawi la Bw Kenyatta ambalo limetangaza kujiunga kwa KANU na muungano wa upinzani ODM likasisitiza kutomtambua Biwott na wenzake, likisema mkutano wao wa Mombasa haukua halali. Wadadisi wanasema hali hii ya sasa inaashiria kumeguka kwa chama cha KANU kilichokua chimbuko la kupigania uhuru wa taifa hilo la Kenya.