1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Wabunge kupata kifuta jasho cha milioni 1.4

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdP

Polisi nchini Kenya wamefyatua gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga kifuta jasho kinachopangwa kupewa wabunge kabla ya muhula wao kukamilika mwezi Disemba.Waandamanaji wanaongozwa na Shirika La Kisheria linalopambana na Ufisadi walijaribu kufika katika maeneo ya majengo ya bunge huku wakipiga mbinja na kubeba mabango yanayopinga hatua hiyo.Wabunge hao wanatarajiwa kupata shilingi bilioni 1.4 za Kenya za ziada kabla uchaguzi kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Polisi walifunga barabara iliyoko nje ya majengo ya bunge na kufyatua gesi ya machozi ili kutawanya kundi la waandamanaji.Viongozi 5 wa maandamano hayo walikamatwa na kuzuiliwa kwenye kituo cha polisi cha majengo ya bunge.

Mwaka 2003 wabunge walijiongezea kiwango cha mshahara kwa mara nne mara tu baada ya kushika wadhifa huo.Chini ya mpango huo mpya endapo mswada huo utapitishwa bungeni wabunge hao wanatarajiwa kupokea asilimia 12 u nusu ya pato la mwaka mzima kuanzia mwaka 2003.