1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAJAF:Watu 250 wauawa Najaf wakati maandalizi ya Ashura yaendelea

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWs

Polisi nchini Iraq wanasema kuwa majeshi ya Iraq yakiungwa mkono na ndege za Marekani wamesababisha vifo vya wapiganaji 250 wa Kiislamu katika mashamba ya matunda karibu na mji mtukufu wa Najaf.Kulingana na gavana wa eneo hilo wapiganaji hao walipanga kushambulia viongozi wa kidini wa Shia hii leo wanapojiandaa kwa sherehe ya kidini ya Ashura,.Ndege za Marekani zililenga eneo hilo la mapigano na kulingana na jeshi la marekani ndege yao moja ilidondoka na kusababisha vifo vya wafanyikazi wake wawili.Makamu wa Rais wa Marekani Dick Cheney aliyezungumza na gazeti la Newsweek anasema kuwa mpango wa Rais Bush wa kupeleka majeshi alfu 20 ya ziada nchini Iraq sharti uendelee huku ghasia zikiendelea.Kauli hiyo inatokea baada ya maandamano mjini Washington ya kupinga vita nchini humo.

Mgombea urais kwa tiketi ya Demokratik Bi Hilary Clinton anatoa wito kwa Rais Bush kuondoa majeshi ya Marekani nchini Iraq ifikapo mapema mwaka 2009 ambao ni mwisho wa muhula wake.