1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namna unavyolala ni muhimu kwa afya yako

Amina Abubakar27 Agosti 2014

Je, unajuwa kuwa usingizi ni muhimu sana kwa afya yako na sio tu muda unaolala bali pia namna unavyolala? Unafahamu kwamba staili zako za kulala na mahala unapolalia pana maana kubwa kwa siha yako?

https://p.dw.com/p/1D1jK
Mama akiwa amelala na mwanawe.
Mama akiwa amelala na mwanawe.Picha: imago/imagebroker

Katika makala hii ya Afya Yako, Amina Abubakar anajadili kwa kina zaidi namna ya kulala na jinsi baadhi ya namna tunazotumia kulala zinavyoathiri afya zetu moja kwa moja. Iwe ni kuumwa viungo vya mwili pindi tunapoamka au kuathiri zaidi afya zetu kwa kuziba mifumo ya hewa na kuathiri mishipa ya fahamu na uti wa mgongo.

Amemualika Daktari Mugisha Nkoroko kuchambua suala hili kwa kina zaidi na pia kuna mtu aliyebadilisha namna ya kulala kutokana na maumivu makali aliyokuwa akipata kila anapoamka.

Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Khelef