1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani achaguliwe kuwa rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani?

Oumilkher Hamidou2 Juni 2010

Juhudi za kumchaguwa atakaeshika nafasi ya Horst Köhler zimeshika kasi-baraza kuu la taifa litakutana June 30 ijayo

https://p.dw.com/p/NfWT
Kansela Merkel akitoa taarifa May 31 iliyopita baada ya Horst Köhler kujiuzulu wadhifa wa rais wa shirikishoPicha: AP

Serikali ya muungano ya vyama vya CDU/CSU na waliberali wa FDP inapanga kumteuwa haraka atakaeshika nafasi ya rais wa shirikisho,baada ya horst Köhler kujiuzulu.Majina kadhaa ya wanasiasa ikiwa ni pamoja na wakuu wa dini yamekuwa yakitajwa.Anaepewa nafasi nzuri lakini ya kuchaguliwa na serikali ya muungano ni waziri wa kazi Ursula von der Leyen.

Atakaeteuliwa kugombea wadhifa wa rais wa shirikisho,jina lake linatakiwa lijulikane kabla ya jumapili ijayo wakati serikali ya muungano ya vyama vya CDU/CSU na FDP watakapokutana kutafakari namna ya kupunguza matumizi.Pengine makundi ya wabunge wa vyama hivyo wakashauriana mapema wiki ijayo kuhusu nani akabidhiwe wadhifa huo.

Duru za kutoka vyama ndugu vya CDU/CSU zinasema kansela Angela Merkel anapendelea zaidi wadhifa huo akabidhiwe waziri wa ajira wa serikali kuu bibi Ursula von der Leyen.

Kansela Merkel ameutetea uamuzi wake huo wakati wa mkutano wa vyama vinavyounda serikali kuu ya muungano mjini Berlin,hapo jana.

Mwengine anaepewa nafasi nzuri ya kuteuliwa kupigania wadhifa huo ni spika wa bunge la shirikisho-Bundetag- Norbert Lammert anaetokea pia katika chama cha CDU sawa na bibi Ursula von der Leyen.

Chama shirika cha FDP ,kwa mujibu wa mkuu wa chama hicho bungeni Otto Fricke hakina mgombea maalum wa kiti cha rais wa shirikisho.Hata hivyo bibi Hildegard Hamm-Brücher ,mwanachama wa zamani wa FPD aliyewahi binafsi kupigania wadhifa huo katika mwaka 1994 kwa tikiti ya chama hicho cha kiliberali amependekeza mwenyekiti wa zamani wa kanisa la kiinjili,askofu mkuu wa zamani wa Berlin,Wolfgang Huber.CDU/CSU na FDP wanahisi wao ndio ahakku wa kumteuwa mridhi wa kiti cha rais wa shirikisho.

Kansela Angela Merkel anasema

"Na kwa namna hiyo nnaamini,tuna nafasi nzuri ya kutoa pendekezo la maana.Tukimpata mtu anaefaa,tutawasilisha pendekezo letu kwa wengine pia."

Serikali ya muungano inajaribu kumpata mtu atakaekubaliwa pia na upande wa upinzani.

Ursula von der Leyen nach Hartz-IV-Urteil
Waziri wa ajira,bibi Ursula von der Leyen anaepeqwa nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuwa rais wa shirikisho la jamhuri ya UjerumaniPicha: AP

Mbali na bibi Ursula von der Leyen,wanasiasa wengine wanaotajwa ni pamoja na waziri wa fedha Wolfgang Schäuble,,waziri wa elimu bibi Annette Schavan na mkurugenzi wa muda mrefu wa zamani wa shirika la Umoja wa mataifa la usafi wa mazingira Klaus Töpfer.

Baraza kuu la taifa,ambalo ni mchanganyiko wa wabunge ,wawakilishi wa baraza la wawakalishi wa majimbo na watu wengineo kutoka sekta tofauti za kimaisha humu nchini,linatazamiwa kukutana June 30 ijayo kwa kikao cha 14 ili kumchagua atakaeshika nafasi ya rais wa shirikisho iliyoachwa kwa ghafla na Horst Köhler.

Mwandishi:Hamidou,Oummilkheir/Reuters,epd/Dpa

Mpitiaji:Mohammed Abdul-Rahman