1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani atasalimika katika kundi la kifo, Kundi B

7 Juni 2012

Imebakia siku moja tu kabla ya kuanza kwa patashika ya kuwania taji la ubingwa wa mataifa ya Ulaya,kombe la UEFA, Euro 2012.Timu16 zilizogawanywa katika makundi manne zitawania taji hilo nchini Poland na Ukraine.

https://p.dw.com/p/159yv
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) unterhaelt sich am Mittwoch (06.06.12) in Sopot bei Danzig (Polen) im EM-Quartierzum der deutschen Mannschaft bei einem gemeinsamen Abendessen mit den Spielern Mesut Oezil (v.l.), Tim Wiese und Sami Khedira. Merkel ist am Mittwochabend zu einem Kurzbesuch bei der deutschen Fussball-Nationalmannschaft in Danzig eingetroffen. Drei Tage vor dem ersten Gruppenspiel bei der Europameisterschaft gegen Portugal kam die Kanzlerin gegen 19.30 Uhr in das Quartier "Dwor Oliwski", das die Auswahl des Deutschen Fussball-Bundes (DFB) am Montag bezogen hat. (zu dapd-Text) Foto: Guido Bergmann/Pool/dapd
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akila chakula cha jioni na kikosi cha UjerumaniPicha: dapd

Kwa baadhi itakuwa ni jinamizi, kwa wengine ni changamoto kubwa mno. Lakini katika suala moja wote wanakubaliana , kuwa kundi B la mashindano haya ni gumu mno. Nchini Denmark watu husema kuwa ni kundi "lenye miripuko", amesema hayo kocha wa kikosi cha Denmark Morten Olsen. Kundi hili linajumuisha timu za Ujerumani, Ureno, Denmark na Uholanzi.

Katika mashindano kama haya mwaka 1992 , Ureno, Uholanzi na Ujerumani zilikuwa katika kiwango cha pekee. Denmark inajiona kuwa haina chake katika kundi hili. Sisi ni wanyonge katika kundi hili. Hatuna nafasi kubwa, amesema mchezaji bora wa mwaka nchini Denmark William Kvist ambaye huchezea timu ya VfB Stuttgart nchini Ujerumani. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw hata hivyo, anaiangalia Denmark kwa njia tofauti kabisa. Wadenmark huingia katika mashindano kama haya bila ya wasi wasi. Hawana woga na timu kubwa ama majina. Hali hii inawafanya wawe hatari zaidi.

Bundestrainer Joachim Löw stellt am Dienstag (29.05.2012) Hütchen auf im Training auf einem Fußballplatz in Tourrettes (Frankreich) in der Nähe von Cannes. Die deutsche Fußball-Nationalmannschaft bereitet sich in einem Trainingslager in Südfrankreich auf die EM 2012 vor. Foto: Andreas Gebert dpa
Kocha wa Ujerumani Joachim LöwPicha: picture-alliance/dpa

Hata Ureno ingependelea kuwamo katika kundi rahisi kidogo. Kwa kuwa Ujerumani na Uholanzi zinaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi katika kundi hili. Hili ni kundi gumu kabisa , likiwa na timu tatu kubwa , ameeleza hayo kocha wa Ureno Paulo Bento.

Ugumu usingepaswa kuwapo, lakini mchezo wa kwanza timu hiyo inapaswa kupambana na Ujerumani. Timu hiyo makamu bingwa wa kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2004 inataka kulipa kisasi kwa kufungwa na Ujerumani katika mashindano yaliyopita ya kombe la Ulaya na kombe la dunia katika mwaka 2006. Ureno inaweza kuwa bingwa wa kombe la mataifa ya Ulaya, anasema nyota wa zamani wa Ureno Luis Figo.

Former soccer player Luis Figo arrives with the Spanish/Portuguese delegation at the FIFA headquarters in Zurich, Switzerland, on 02 December 2010. Photo: Hubert Boesl
Mchezaji nyota wa zamani wa Ureno Luis FigoPicha: picture-alliance/dpa

Mara baada ya kupambana na Ureno , Ujerumani haitapumua kwani inakabiliana na mahasimu wao wa jadi Uholanzi. Tunajiamini , amesema kocha Löw. Wachezaji wanajisikia kuwa wako karibu na mafanikio makubwa. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel siku ya Jumatano(06.06.2012) alikula chakula pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani siku tatu kabla ya kupambana na Ureno , katika Hotel Dwor Oliwski mjini Dazig nchini Poland. Merkel amesema kuwa nimehisi na kugundua kuwa kuna mshikamano na ari kubwa miongoni mwa wachezaji.

"Nimefurahi kwamba nimeweza kuja kuwatembelea . Nafahamu kuwa muda wa matayarisho kwenu mwaka huu umekuwa mfupi sana na natambua kuwa hilo mmelitilia maanani".

Kwa kupata matokeo mazuri katika michezo kumi ya kuwania kufuzu kucheza katika fainali hizi, timu hii inataka kutawazwa bingwa wa taji hili ambalo walilitwaa mwaka 1972, 1980 na 1996.

Dutch national team soccer coach Bert van Marwijk observes his team during the first training session of the Netherland's national soccer team in Lausanne, Switzerland, Friday, May 18, 2012. Netherlands National Football Team is in Lausanne for a training camp in preparation for the UEFA EURO 2012 soccer championship, hosted jointly by Poland and Ukraine. (Foto:Keystone/Laurent Gillieron/AP/dapd)
Kocha mkuu wa Uholanzi Bert van MarwijkPicha: dapd

Uholanzi nayo inataka ubingwa wa kwanza baada ya miaka 24. Mwaka 1988 Uholanzi ilitawazwa bingwa wa mashindano haya,na tangu wakati huo Uholanzi haijafika hata katika fainali. Kikosi hicho chenye kiu kubwa ya kupata mabao cha kocha Bert van Marwijk kimefanikiwa bila matatizo kuingia katika fainali hizi na kupata mabao 37, manne zaidi ya magoli yaliyofungwa na Ujerumani katika hatua hiyo. Mstari wa ushambuliaji unaongozwa na Klaas-Jan Huntelaar na Robin van Persie. Lakini pamoja na hao wako nyota kama Wesley Sneijder, Arjen Robben na Dirk Kurt. Pamoja na kuwa na kikosi cha mauaji, lakini kocha van Marwijk anaheshimu timu katika kundi hili lenye miripuko.

Mwandishi : Olivia Fritz / ZR / Kitojo

Mhariri: Othman Miraji